Hadithi: SITASAHAU YALIYONIKUTA BAADA YA KUMSOMESHA MPENZI WANGU ????????.
Mtunzi:Mwaki Ze Done(0653814440)
Sehemu Ya 1 & 2
Ilikuwa ni Tarehe 25 kwenye mwezi wa kumi na Moja kama sijakosea, Mimi na Rafiki Yangu Muba tulikuwa tumesafiri kutoka Morogoro Wilaya Ya kilosa Maeneo Ya Dumila mpaka Mbeya, na Lengo la kwenda Mbeya Ilikuwa ni Mahafari Ya Chuo kikuu Cha Mzumbe kilichopo Mbeya, ilikuwa ni Mahafari ambayo Mpenzi Wangu Frida ambaye huwenda nilimpenda kuliko Nilivyo jipenda Mimi alikuwa anasherehekea kuhitimu masomo Yake Mara baada ya kusomea Shahada Ya Uongozi wa Umma (Bachelor of Public Administration) Kwa Miaka Mitatu.
Siyo kwamba Frida alikuwa kanialika Labda kwamba niende ama Laaa, ila alikuwa amenipa taarifa tu kwamba Kuna Mahafari, Basi Mimi na mwanangu Muba katika kushauriana tuliona itakuwa vyema endapo tutasafiri kwenda kumuunga Mkono kwenye Sherehe Hizo, Maana Hata Hivyo asilimia kubwa mpaka Frida anafika levo ile Mimi Ndo nilikuwa nimegharamia.
Siku zote Siku mbaya Dalili Zake huonekani asubuhi, na Dalili ya Mvua Siku zote ni Mawingu, Kwanza nakumbuka Siku Hiyo Dalili mbaya naweza Sema zilianzia Toka kwenye Gari, maana Siku hiyo tunasafiri kwenda huko Mbeya Ndo Siku ambayo Hata Dada Yake na Frida pamoja na Bibi Yake walikuwa nao wanasafiri na tulijikuta tunapanda Gari Moja Wote pasipo kujua!.
Na Dada Yake Frida alipo niona aliniuliza naenda Wapi, basi Jibu nililo mpatia ni kwamba wanako elekea na Mimi ndo huko Huko naenda, Lakini baada ya Jibu Hilo kiukweli safari nzima Dada huyo pamoja na Bibi Yake walikuwa wanatuangalia vibaya Muno yaani kama wana chuki na Sisi au hawajapenda kabisa Sisi kwenda huko kwenye Mahafari!.
"Oyaa!! Baloteli mwanangu una uhakika kabisa Frida atafurahia Sisi kuwepo huko kwenye Mahafari, maana naona Fina na Bibi Yake wanatuangalia vibaya Muno!"
"Oyaa Muba we Kausha Hata usiwaangalie! Mimi Najua Frida ananipenda na hawezi kwazika Kwa Mimi kwenda kwenye Mahafari Yake, kwanza itakuwa kama surprise naamini atafurahia Muno kuniona!"
"Daaaaaaa!! Sema haina noma Frida namuaminia ila Duuuuuu huyo mbibi na Fina wanavyo twangalia Sasa kama hawajafurahi hivi kutuona!"
Hayo yalikuwa mazungumzo Yangu Mimi na mshikaji Wangu Muba!.
Basi Safari ile ilikuwa ya masaa kadhaa, nakumbuka Mbeya tuliingia Mida ya Saa Kumi na Moja za Jioni, Lakini Dalili mbaya zilizidi zaidi kuonekana baada ya kufika Stendi Kuu ya Mbeya!.
Baada ya kushuka tu kwenye Gari nilimuona Fina na Bibi Yake wanaangaza Huku na Kule kana kwamba wanamuangaza Mtu ambaye kaja kuwapokea, ni kweli baada ya dakika kadhaa niliwaona wakibeba mabegi na kuelekea taxi zilipo, nilipo piga Macho Kwa mbali nilimuona Frida akiwa na Rafiki Zake kama wawili hivi, kwanza Macho Yangu na Macho ya Frida viligongana baada ya Hapo Frida alikwepesha macho na kujifanya hajaniona.
Fina na Bibi Yake walipokelewa mabegi na Frida baada ya Hapo Wote Kwa pamoja walizama kwenye taxi na kuondoka, kiukweli nilijisikia vibaya Muno, niliamini huwenda Frida Hajaniona kama ni Mimi Ndo maana kapotezea, kwanza sikutaka Hata kumshirikisha Muba kile kitendo, maana mchizi Wangu alikuwa ni Mtu wa maamuzi magumu, huwenda ningemwambia pale pale angenambia tugeuze turudi!.
Mimi na Muba Wote tulikuwa Wageni kabisa ndani ya Jiji la Mbeya, yaani hakuna ambaye alikuwa amewahi kufika, basi ilibidi tuulize Chuo Cha Mzumbe kilipo, Waungwana walituelekeza vizuri kabisa na walitushauri tupande Bodaboda maana Kwa Mguu ni mbali kidogo!.
Ni kweli Mimi na Muba tulipanda bodaboda mpaka Maeneo Ya Forest ambako Ndo chuo Cha Mzumbe kilipo, ilikuwa ni kama Saa Kumi na Mbili na madakika hivi, kigiza kilikuwa kimeanza kuchanganya Huku kibaridi nacho kikiwa Cha kutosha!.
Kwakuwa Mahafari yenyewe ilikuwa Siku ya Kesho Yake, ilibidi Mimi na Muba tutafute sehemu ya kulala Kwa Siku Hiyo na kweli kuna Guest karibia na maeneo ya chuo tuliipata!.
Sasa baada ya kuwa nimetulia Majira ya usiku niliamua nimpigie kipenzi Changu Frida ili nimpe taarifa,Japo nilikuwa naamini lazima Dada Yake na Bibi yake wamempa taarifa, Lakini nilitaka na Mimi nimwambie kivyangu!.
Kiukweli nilipiga Simu Siku hiyo mpaka Simu yenyewe Nahisi ilinichoka, yaani nilipiga Simu mpaka Ilianza kupata Moto, Frida hakupokea Simu Yangu Hata Mara Moja, Mwishowe Simu iliacha kupatikana!.
Kiukweli nilijikuta Mwili mzima umeanza kutoka Jasho, yaani na baridi lote la Mbeya Lakini Mimi nilikuwa natiririkwa na Jasho la kutosha, kwanza Hasira ambayo nilikuwa nayo ilikuwa Juu Muno!.
Mpenzi Msomaji Najua unajiuliza Nilikuwa najiamini Nini mpaka kuja kwenye Mahafari pasina Hata kualikwa na kwa Nini nilikuwa na hasira, Ngoja nikurudishe Nyuma kidogo, hakika Hii ni Huzuni huwenda ukatokwa na Machozi kabisa.............
Mimi naitwa Jupita Matandu ni Mzaliwa wa Kilosa Maeneo ya Dumila, Kwa Baba na Mama tulizaliwa wawili tu, Mimi na mdogo Wangu wa Kike anaitwa Febi!.
Nilisoma Shule ya Msingi Dumila na baada ya kumaliza Darasa la Saba nilifanikiwa kujiunga na Sekondari ya Dumila! Hapo Ndipo nilipo kutana na Binti aliye Julikana Kwa Jina la Frida, kiukweli Frida alikuwa ni Binti mwenye akili Muno pale Shuleni, na akili Zake zilifanya Mimi niwe najipendekeza kwake ili awe ananifundisha fundisha!.
Ni kweli baada ya kufika kidato Cha Pili urafiki Wangu na Frida ulizidi kuwa mkubwa na kilicho Fanya urafiki wetu kuwa mkubwa ni kwamba Mimi nilikuwa Masta wa kucheza Mpira, yaani nilikuwa nacheza Mpira kuliko Kawaida kiasi kwamba Shule za jirani wakiambiwa wanacheza na Shule yetu wote walikuwa wananiwaza Mimi, Yaani nilikuwa fundi kiasi kwamba nilipewa Jina la Utani la Baloteli ambalo Mwishowe Ndo lilikuja likavuma zaidi kuliko Hata Jina Langu la Jupita.
Basi tulivyo Fika kidato Cha Tatu Kwa bahati mbaya Mama Yake na Frida alifariki Dunia, na Mama huyo Ndo alikuwa kila kitu Kwa Frida maana Baba Yake na Frida alikuwa ashafariki Muda Sana!.
Baada ya Mama Frida kufariki maisha ya Frida yalianza kuwa magumu Muno, maana ilibidi Frida na Dada Yake Fina waanze kulelewa na Bibi Yao ambaye naye alikuwa hajiwezi kila kitu!, Dada Yake na Frida ambaye ni Fina ilibidi aache Shule ilimladi aweze kufanya vibarua kusaidia familia! Na Dada Yake Huyo aliacha shule akiwa kidato Cha Nne, na ilikuwa Rahisi kuacha Shule Kwa sababu hata hivyo Fina alikuwa akili za Darasani Hana, yaani walikuwa ndo wale wanaosindikiza wenzao Shuleni, aliona ni Bora aache ili amsaidie mdogo Wake Frida ambaye huwenda alikuwa na akili Shule nzima!.
Basi maisha yaliendelea tukiwa tumemaliza kidato Cha Tatu kuingia Cha Nne, baadhi ya Rafiki Zangu walinishauri nimtongoze Frida, kama tujuavyo marafiki wanavyo juaga kujaza maneno!.
"Oya Baloteli unakwama wapi, Demu anaonekana anakuzimikia kabisa yule, Wewe tupia nyavu!"
"Tuna uhakika yule hawezi kuruka kamba!"
Hayo ni baadhi ya maneno ya ujazo kutoka Kwa washikaji Zangu, na kweli maneno hayo yalifanya nivimbe kichwa na kumtongoza Frida!.
Kiukweli mwanzo Frida aligoma Kwa Msisitizo Muno kwamba Yeye hajafuata Mapenzi Shuleni Bali masomo, Lakini baada ya Frida kushauliwa na Dada Yake Fina aliamua kunikubalia, niligindua tu Fina kamshawishi mdogo Wake anikubalie Kwa sababu ya vimali vya nyumbani, maana kiukweli nyumbani tulikuwa tunajiweza Japo Siyo Sana!.
Mapenzi Moto Moto yalianza kati Yangu Mimi na Frida, kiukweli nilitokea kumpenda kupita kiasi, yaani Muda Wote nilikuwa nasafiri mpaka Kijiji Cha Pili Kwa kina Frida.
Hatimaye tulimaliza kidato Cha Nne, Hapo Ndo mapenzi yalizidi kuwa Moto Moto Mara baada ya kuonja Tamu ya Frida na nakumbuka Mimi Ndo nilikuwa Mwanaume Wake wa kwanza kumuonja. Yaani asubuhi na mapema nilikuwa nawahi kuondoka nyumbani mpaka Kwa Bibi Yake na Frida.
Nilijikuta nimeacha kufanya Kazi nyumbani badala yake nikawa nafanya Kwa kina Frida!.
Yaani nyumbani kulikuwa na mashamba kibao ya kulima, Lakini nilikuwa nawahi kulima Kwa kina Frida, kitendo hicho kilifanya Baba Yangu kunigombeza Muno na kutishia kunifukuza nyumbani.
Basi miezi kadhaa ilipita, baada ya matokeo kutoka kiukweli nilifurahi Muno, Siyo kwamba nilikuwa nafurahi Kwa sababu nilikuwa nimefaulu Bali furaha Yangu ilikuwa ni kuona Frida kafaulu kwenda kidato Cha Tano!.
Mimi nilifeli tena vibaya Muno, Lakini wala sikuumizwa na kufeli Kwangu Kwa sababu niliona kufaulu Kwa Frida Ndo kufaulu Kwangu!.
Basi baada ya Muda kupita Frida alipangiwa kwenda kusoma Songea Girls iliyopo Songea mkoa wa Ruvuma.
Kiukweli ilikuwa changamoto Kwa familia ya kina Frida kumudu Gharama, maana mahitaji yalikuwa mengi, pia changanya nauli na Gharama zingine.
Dada Yake na Frida alikuwa ni Mtu mjanja mjanja wa maneno matamu, basi Kwa sababu Yeye Ndo alikuwa kama kichwa Cha familia aliamua kunifuata Siku Hiyo kunipangilia.
"Baloteli najua unampenda Muno mdogo Wangu, na unajua Wewe Ndo utakuwa Mume wake wa maisha Yake, na mdogo Wangu anavyo kupenda mpaka Usiku huwaga anataja Jina lako akiwa usingizini, najua mdogo Wangu akifanikiwa na kupata maisha mazuri atakaye faidika zaidi ni Wewe! Kwa Hiyo kitu ambacho nakuomba jitahadi ufanye Namna tupate pesa Frida aende Shuleni, Mimi hapa nilipo ninayo Tsh elfu hamsini tu, na nimepiga mahesabu ni Kama Tsh Laki Tatu zinahitajika!" Hayo yalikuwa maneno matamu ya Fina, kiukweli nilijisikia fahari Muno kusikia mtoto Frida huwaga ananiota usiku, Japo kuwa nilikuwa sina Kazi Yoyote ya kuniingizia kipato ila nilimuahidi Fina kwamba hiyo Pesa ntaipata tu!.
Basi Siku zilisogea hatimaye Sasa ule Muda ambayo ilitakiwa Frida asafiri kwenda Shule ulifika! Kiukweli nilikuwa sikubali kabisa kuikosa pesa ya kumpatia Frida!.
Nakumbuka pale nyumbani palikuwa na Duka la matumizi ya Nyumbani, Siku Hiyo wazazi Wangu wakiwa shambani niliamua kuingia Dukani kiwizi wizi, maana nilikuwa nimekatazwa kabisa kuuza Duka, Bali mdogo Wangu Febi Ndo alikuwa anaruhusiwa tu.
Mwanaume nikiwa sijali nilivuta Droo kwenye Duka na nilibeba Pesa zote ndani ya Droo, baada ya Hapo nilizunguka upenuni kuzihesabu, zilikuwa kama TSH elfu 80 hivi, niliona hiyo haitoshi, nilizama Tena ndani niliamua kuingia chumbani Kwa Wazazi Wangu, nilipekenyua mpaka nilipata wanapo hifadhi Pesa!.
Nilichukua Pesa Zote ambazo nilizikuta, nakumbuka zilikuwa zimewekwa kwenye kisado kidogo alafu zikawekwa Chini ya kitanda!.
Baada ya kuhesabu Zile Pesa nilikuta zipo kama Laki mbili na Nusu Hivi changanya na ile ya Dukani zilikuwa zinatimia kama Laki Tatu na kitu.
Basi nilichukua Laki na Nusu na kuiweka pembeni, zile zilizo bakia nilizibeba ili nikarudishe chumbani ili nisije shitukiwa Sana!.
Bahati mbaya Wakati nataka kurudisha nilikuta Wazazi Wangu wamerudi Kwa hiyo nilishindwa kuzirudisha!.
Baada ya Hapo nilielekea mpaka Kwa kina Frida, nilimpatia Frida pesa zote, yaani hata Zile zingine Nazo nilimpatia Huku Bibi Yake na Dada yake wakinisifu Muno kwamba Mimi ni kijana mwenye Upendo mkubwa na Bila Shaka ntamuoa mtoto Wao!.
Siku Hiyo nilirudi nyumbani majira ya Saa Tatu Usiku, niliulizwa kuhusu Pesa zilizo potea Dukani kiukweli nilibisha Muno Siku Hiyo na bahati mbaya au nzuri Bado walikuwa hawajaangalia hata chumbani kama Nako Pesa zimeibiwa, kwakuwa kulikuwa hakuna ushahidi niliponea chupu chupu!.
Basi baada ya Siku mbili Frida alisafiri kuelekea Huko Shuleni na Mimi nilbaki nakenua tu Meno nikijiona shujaa!.
Baada ya Siku kama mbili Hivi Baba aligundua kwamba Pesa Zake kwenye kisado zimeibiwa, Hakika Siku Hiyo Baba aliwaka Muno yaani Mimi na mdogo Wangu tulipigwa kipigo Cha mbwa Koko, Lakini tulikataa kutoziona zile Pesa na pia Mama alisaidia kututetea kwamba hatuna tabia ya Wizi Bali huwenda kuna Mwizi alikuja.
"Okay Sasa nimechoka kuibiwa, Awamu hii lazima niende Kwa mganga, atapatikana tu aliyeziiba!" Hiyo ilikuwa Kauli ya Baba akiwa na hasira, kiukweli Kauli hiyo ilifanya Macho yanitoke kama nimedungwa na sindano matakoni!.
Je ipi hatima ya Kijana Baloteli au Jupita!? Kwa nini anasema hatasahau, yapi yalimkuta!?? Usikose uhondo Huu!.
Tukutane sehemu ya 2
Hadithi: SITASAHAU YALIYONIKUTA BAADA YA KUMSOMESHA MPENZI WANGU ????????.
Mtunzi:Mwaki Ze Done(0653814440)
Sehemu Ya 2
"Okay Sasa nimechoka kuibiwa, Awamu hii lazima niende Kwa mganga, atapatikana tu aliyeziiba!" Hiyo ilikuwa Kauli ya Baba akiwa na hasira, kiukweli Kauli hiyo ilifanya Macho yanitoke kama nimedungwa na sindano matakoni!.
Yaani nilijikuta Mwili mzima umeanza kutetemeka mpaka Baba na Mama walianza kunishangaa, Mtu mzima ni Mtu mzima tu na huwezi shindana na Mzazi Mbinu!. Baba ni kama aligundua kwamba Mimi Ndo mhusika Kwa Nilivyo kuwa natetemeka yaani Hapo Ndo alizidisha vitisho!.
"Yaani yule Bibi ambaye nataka kwenda hajawahi kosea, yaani Huyo Mwizi aliye Iba hatafika Kesho lazima afe na asipo kufa lazima awe kichaa muokota makopo! Mama Febi niandalie Nguo Zangu niende Muda Huu!" Baba alizidi kuchimba mkwara akionekana yupo serious, Hakika nilichanganyikiwa Muno, nilifikiria kwamba Ndo naenda kufa na nimuache mpenzi Wangu Frida hivi hivi, niliona hiyo haiwezi tokea.
Kabla Baba Hata hajanyanyuka niliamua kuropoka kwamba ni Mimi niliiba!.
Kwa Mara ya kwanza Siku Hiyo nilijiharishia Kwa kipigo nilicho pewa na Baba, yaani mpaka Mama alianza kuingilia, kiukweli Baba alinipiga Muno Siku Hiyo, kutokana na kipigo kile niliropoka kila kitu Mpaka niliko peleka Pesa!.
"Kwakuwa ushakuwa Mtu mzima na Wewe umeanza kusomesha mpaka wanawake, Sasa nakuomba Hapa Kwangu uondoke nisije kukuona unatia Mguu tena hapa Kwa lolote!" Baba alitamka maneno Hayo akiwa na hasira Muno, na kweli ilibidi nikimbie pale nyumbani maana kipigo bado kilikuwa kinaendelea!.
Kuanzia Siku Hiyo Kwa Mara ya kwanza nilianza kujitegemea na Ndo Siku ambayo Mimi nilianza kuishi na Rafiki Yangu Namba Moja Bwana Muba!.
Muba alikuwa ni Yatima ambaye wazazi wake walifariki Kwa ajali, na Muba alikuwa kaachiwa nyumba na wazazi Wake na alikuwa anaishi pekee Yake, Kwa Hiyo baada ya kutimuliwa pale nyumbani, rasmi nilianza Kuishi Kwa kina Muba!.
Mimi na Muba tulikuwa Watu wa Vibarua tu, yaani ilikuwa Sisi na vibarua.
Pesa zote ambazo nazipata zilikuwa zinaishia Kwa kina Fina, maana kila Muda Fina alikuwa ananifuata kutaka Pesa za kumtumia Frida Shuleni, Kwa Hiyo nilijikuta kila Senti ninayo ipata inapitiliza Kwa Frida!.
Mwaka mzima ulipita nikiwa napambana, Frida alirudi likizo basi alionesha kunijalia na kunipenda Muno, yaani Hapo Ndo nilikuwa napagawa kabisa!.
Basi Siku hazingandi, Frida alirudi Shuleni kumalizia kidato Cha Sita huku Mimi nikiwa Ndo Jicho lake la Pesa!.
Kipindi hicho Mimi na Muba tulikuwa tumeanza kufanya biashara ya kutembeza Nguo za mtumba, yaani tulikuwa tunaagiza Mzigo wa mitumba alafu tunasambaza.
Kiukweli biashara ile ilikuwa inatulipa vizuri, wakati rafiki Yangu Muba anaweka Pesa Zake Mimi nilijikuta zinaishia kwenye familia ya Kina Frida!.
Muba alinunua mashamba Kadhaa kupitia ile biashara, Lakini Mimi hakuna ambacho nilikuwa namiliki, Japo Muba alijaribu kunishauri Lakini linapo fika Swala la Frida kiukweli nilikuwa sitaki ushauri Hata kidogo!.
Ilifika kipindi Muba baada ya kuona nimezidi aliamua kwenda Kwa wazazi Wangu kunisemelea.
Japo Baba alikuwa kanitimua nyumbani Lakini Bado uchungu wa kama mzazi ulikuwepo, Baba aliamua kuniita nyumbani na kweli nilipo enda Yeye na Mama walinikarisha Chini!.
Kiukweli Siku hiyo niliwajibu shombo Muno wazazi Wangu mpaka Leo huwaga nakumbuka!.
Baada ya kuwajibu shombo niliondoka Kwa hasira pale nyumbani, na nilipo fika tulipo kuwa tunaishi Mimi na Muba nilimfokea Sana Muba Kwa umbea alio upeleka Kwa wazazi Wangu.
Basi Siku Nazo hazingandi hatimaye, Frida alimaliza kidato Cha Sita, na Mwisho wa Siku matokeo yalitoka vizuri kwamba amefaulu inatakiwa aende Chuo!.
Ndugu Msomaji huwezi Amini nilikuwa nafurahi kana kwamba Mimi Ndo nimefaulu Hivi, yaani nilikuwa naona maisha ya Frida ni maisha Yangu Mimi!.
Miezi kadhaa Frida alipata majibu kwamba inatakiwa akajiunge na Chuo kikuu Cha Mzumbe kusomea maswala ya uongozi na bahati mbaya kuliko zote, Frida alipata Mkopo asilimia chache tu, Kwa Hiyo ilikuwa inahitajika Pesa nyingine ya kuongezea!.
Kiukweli naweza Sema mapenzi yaliniweka upofu, nakumbuka kipindi hicho ulikuwa Ndo Muda Ambao Frida alitakiwa aende kuanza chuo, na Pesa kama Laki nane ilikuwa inatakiwa, kiukweli kipindi hicho nilikuwa sina Pesa maana Mimi na Muba tulikuwa tumepumzika biashara na tumewekeza kwenye kilimo.
Mimi na Muba tulikuwa tumelima matikiti karibia hekali mbili!.
Basi Kitu nilicho kifanya baada ya kuona Sina Namna ya kupata Pesa Hizo, niliamua kumtafuta mteja kimya Kimya tena Kwa Bei ya Hasara, Wakati Muba hana Hata taarifa niliamua kwenda kuvuna Matikiti karibia shamba Zima na Fuso ilipakia mpaka Juu!.
Basi nilipewa Million Moja Keshi na yule niliye mjumulishia Yale Matikiti, pesa Yote kama ilivyo nilienda kumpatia Frida ili aende Chuo, Kwa kipindi hicho nilikuwa najiona shujaa kweli!.
Muba alikuwa hana taarifa yoyote kuhusu kile nilicho kifanya, maana Hata shamba ambalo tulikuwa tumelima lilikuwa Mbali kidogo na tunako kaa!.
Basi baada ya Siku mbili Frida alienda Chuo Huku tukiwa tumeahidiana Mambo matamu matamu, yaani mpaka Dada yake Fina pamoja na Bibi Yake walikuwa wanajua Mipango yetu!.
Wiki Moja ilipita Huku Muba akiwa hana taarifa kabisa kwamba nimevuna Matikiti Yote, na bahati mbaya kuliko zote yale Matikiti tulikuwa tumelima kwenye Shamba ambalo Muba alinunua kipindi Cha nyuma Wakati tunauza mitumba!.
Baada ya Wiki Kama mbili Muba alinitaka tutafute wateja tukavune Matikiti au kama inawezekana tukodi Gari tusafirishe Mpaka Dar es Salaam, maana kipindi hicho Dar es Salaam kulikuwa na soko Zuri la Matikiti.
Kiukweli nilimzungusha Muno Muba, yaani kila akiniletea habari za Kwenda kuvuna Mimi nilikuwa namkwepa, Mara nitoe sababu ambazo hazieleweki!.
Muba Sijui alipata machare Gani aliamua kwenda Shambani kutembelea na alikuta karibia robo Tatu imevunwa hakika Muba alikasirika, yaani nilikuwa sijawahi kumuona Muba kakasirika kama alivyo kasirika Siku ile, maana aliamua kunitimua mpaka nyumbani Kwao!.
Nilitimuliwa kipindi ambacho nilikuwa sina Hata Senti mbovu, kiukweli nilihaha Muno, nilitamani nirudi nyumbani Lakini nilikumbuka majibu ya shombo ambayo niliwatamkia wazazi Wangu niliona haiwezekani Mimi kurudi nyumbani.
Basi nilifanya maamuzi ya kwenda Kijiji Cha Pili Kwa Bibi Yake na Frida Huko Ndo nilianza kuishi!.
Nilikaa pale Kwa Bibi Yake na Frida kama Wiki mbili hivi Huku nikiwa nasaidia kazi za kilimo pale nyumbani.
Baada ya kukaa hizo Wiki mbili nilipata taarifa kwamba Muba anaumwa Muno na hana Mtu wa kumuuguza, Hapo ilibidi Sasa nirudi tena pale Kwa kina Muba na urafiki wetu ulianza upya, maana nilimuuguza Muba Kwa Upendo mkubwa Muno mpaka alipona na kuwa Sawa.
Basi maisha yaliendelea Huku Siku zikiwa zinakatika! Kiukweli mishe zilikuwa ngumu Muno, Lakini Mimi nilijikuta nimekuwa Mtu wa kucheza Ndondo za kulipwa, yaani kiukweli kwenye upande wa Mpira nilikuwa vizuri Muno! Kwa Hiyo kila Timu jirani za maeneo yale zikiwa na mechi au ligi walikuwa wananikodi Mimi na kunilipa!.
Nilikaa Mwaka mzima nikiwa nimewekeza nguvu kubwa kwenye kucheza Mpira, Lakini niliona kama napoteza Muda hivi, baada ya Muba kunishauri ilibidi Mimi na Yeye tuungane Sasa kwenye biashara ya Nguo tena!.
Kiukweli tulikuwa tunadhurura Muno, yaani tulikuwa tunatembea kuliko Kawaida kuzungusha Nguo, na kila Senti ninayo Pata ilikuwa inapitiliza Kwa Frida.
Basi ilipita Miaka Mwili Huku biashara ya Nguo ikiwa Ndo Kazi yetu ambayo tumeamua kujiwekeza Mimi na Muba na Ndo kipindi hicho Frida alikuwa amemaliza Chuo, na Tangia Frida aanze Chuo alikuwa hajawahi kurudi nyumbani hata likizo Moja! Kwa Mimi na Frida ilikuwa ni kutumiana picha tu!.
Basi kipindi hicho Wakati Frida kamaliza Chuo nilimuuliza Fina kwamba Frida lini anarudi kiukweli Majibu ya Fina yalikuwa ya mkato Muno! Nilienda mpaka Kwa Bibi Yake wanako ishi mapokezi niliyo pokelewa Siku hiyo kiukweli yalikuwa ya tofauti na Siku zote ambazo nilikuwa naenda, yaani walionesha kama hawajafurahishwa na Mimi kwenda pale.
Mimi sikujali nilicho kuwa naamini ni kwamba napendwa na Frida!.
Basi ulipita mwezi mmoja Huku mawasiliano Yangu Mimi na Frida yakiwa yameanza kuwa ya kusuwa Suwa, maana alikuwa hapokei Simu Kwa wakati, SMS hajibu Kwa wakati tofauti na mwanzo!.
Baada ya Muda kupita ukiwa mwezi wa kumi na Moja kwenye tarehe kumi na kitu Frida alinitumia sms kwamba Mahafari Yake ipo Tarehe 26! Kiukweli nilifurahi Muno nilimpigia Simu Frida ni kweli alipo pokea alinithibitishia kwamba Mahafari ipo Tarehe 26!.
Nilijaribu kumuuliza Frida Kwa Mahaba kwamba anahitaji Zawadi Gani kwenye Mahafari Yake Lakini badala ya kujibu alikata Simu, na tokea Siku hiyo Frida alikuwa ananikwepa kwepa, yaani mawasiliano yalikuwa ya nadra mpaka inafika Tarehe 25 ya mwezi wa Kumi na Moja Mimi na Frida tulikuwa tunawasiliana kama Siyo wapenzi Hivi!.
Na Hiyo Siku Ndo nilichukua maamuzi ya kusafiri kuhudhuria Mahafari Huku rafiki Yangu Muba akiwa ameamua kunipa kampani!.
Nadhani ndugu Msomaji umeelewa ilikuwaje mpaka Mimi nikasafiri mpaka Mbeya kuhudhuria Mahafari Bila hata kualikwa.
Tuendeleee Sasa.....
Basi baada ya Frida kunizimia Simu Usiku huo Bwana Muba alinituliza na kunitia Moyo maana nilikuwa na Hasira Muno!.
Tulilala pale Guest House mpaka asubuhi! Hatimaye ilikuwa Siku nyingine, Siku ambayo Ndo Mahafari yenyewe!.
Kiukweli nilijitahidi kupendeza Muno Siku Hiyo maana tayari nilikuwa nimeandaa Nguo maalumu Kwa ajili ya Sherehe!.
Asubuhi ile nilijaribu kumpigia Simu Frida Kwa Mara nyingine Lakini Simu iliita tu pasina kupokelewa!.
"Oya Baloteli usipaniki Kaka, huwenda yupo Bize na maandalizi si unajua maswala ya Sherehe! Heka heka zinakuwa nyingi!" Basi Muba aliongea maneno ambayo yaliendelea kunitia Moyo!.
Nilimpigia Fina Sasa ambaye Ndo Dada yake ili walau anipe utaratibu, Lakini Fina hakupokea Simu Yangu zaidi ya Mara Nne, Mara ya Tano alipokea tena akionekana ana jaziba Muno!.
"Eheee unasemaje!? Maana naona unapiga Simu kama unanidai hivi!?" Hayo ni Maneno ambayo Fina aliongea Kwa Hasira!.
"Samahani Fina Mimi sielewi chochote naomba mnipe basi utaratibu wa Sherehe upoje na mko Wapi!?" Mwanaume nikiwa mnyonge niliuliza Kwa Ustaarabu kabisa!.
"Tukupe utaratibu umealikwa!??" Fina aliniuliza Swali gumu ambalo lilifanya mdomo Wangu uwe mzito, yaani nilihisi kama shoti imepita mwilini Mwangu shwaaa!!!. Siyo lile Swali la Fina ambalo lilifanya nipate kiwewe Bali ni Sauti ya pembeni ambayo niliisikia Kwa mbaali na ilikuwa Sauti ya Frida.
"Muulize kwamba amealikwa!!?" Hiyo Ndo Sauti ambayo niliisikia inamnong'oneza Fina Kwa pembeni na kweli Fina akaniuliza.
Baada ya Hapo Fina alikata Simu baada ya kuona nipo kimya Kwa lile Swali lake!.
"Oya Baloteli hili dharau Mwanangu kama Vipi turudi Moro! Yaani Fina Ndo wakukujibu hivyo! Alafu Nahisi wapo na Frida maana wakati unaongea naye nimesikia Sauti Kwa mbaali ni kama ya Frida!." Baloteli aliongea Kwa jaziba, maana mshikaji Wangu alikuwa hapendi unyonge kabisa, Lakini Mimi niliona Hapana haiwezi kuwa kama Ninavyo waza!.
Basi Mida ya Saa Nne tukiwa tumependeza Mimi na Muba tuliwasili pale Chuo Cha Mzumbe! Kiukweli palikuwa na pirika pirika nyingi Muno Watu walikuwa wamependeza ni hatari, nilijaribu kumuangaza Frida wala sikumuona!.
Mimi na Muba tulizidi kujizungusha Huku na Kule tukiwa tunashangaa tu! Lakini Gafla Muba alinishitua na kunionesha kitu, nilipo angalia Kwa mbaali nilimuona Frida akiwa anashuka kwenye Gari la kifahari, baada ya hapo Bibi Yake na Frida pamoja na Fina nao walishuka!, Mtu ambaye alikuwa anaendesha Gari sikumuona vyema.
Basi nikiwa na tabasamu mwanana niliamua kuwasogelea pale walipo shukia!.
"Wawoooo!! Frida kipenzi umenogaje!!" Basi nikiwa nasogea niliongea kwa furaha Meno Yote yakiwa Nje!.
"Baloteli unafanya Nini hapa!? Au nani kakuita!??" Dada Mtu ambayo ni Fina aliniuliza Swali Kwa jaziba, yaani kama nina ugomvi naye, kabla Hata sijajibu, yule Bwana ambaye alikuwa anaendesha lile Gari la kifahari baada ya kwenda kulipaki ilipo parking alikuja pale tulipo.
"Bebii!! Vipi huyu nani Tena mnajuana!?" Yule bwana ambaye alikuwa kavaa Suti nyeusi ya kaunda aliuliza!.
"Hapana Kipenzi, Huyu tulisomaga naye Shule ya Msingi Ndo Nashangaa nakutana naye leo ni Mtu wa nyumbani kabisa!" Frida akiwa anajichekesha alimjibu Yule Bwana! Kiukweli ndugu Msomaji haya Mambo yasikie tu Kwa mwingine, yaani nilihisi kama nimesimama Juu ya tanuri lenye moto mkali, yaani kwapa zililowa Jasho gafla nilihisi mwili mzima unawaka Moto!
Ndugu Msomaji Hapa Sasa Hadithi Ndo inaenda kuanza!? Na tutajua yaliyo mkuta Baloteli mpaka akasema hatosahu, huo ulikuwa utangulizi tu. Hadithi Haina season ni Single Fully, Mpaka Mwisho TSH 1000 tu OFA.
Namba Za Malipo
Mpesa:0742138331(Madaraka Mwakipesile
Mixx By Yas:0653814440(Madaraka
Whatsapp No:0653814440
Tukutane Sehemu Ya 3.