Ligi Kuu imeendelea kupiga hatua kubwa katika maendeleo kiasi cha kushika nafasi ya nne kwa ubora barani Afrika kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS).
.
Hili ni jambo la kujivunia, lakini uwepo wa watu wanaoitwa makomandoo ambao wamekuwa na jukumu la ulinzi kwa timu husika ni tatizo kubwa ambalo halifai.
.
Tukio la juzi kwamba makomandoo wa timu moja wanadaiwa kuhusika katika kuvuruga na kuathiri kanuni za ligi lina paswa kuwa ishara kwamba, hawa watu hawafai na hawastahili kukumbatiwa na timu hizi mbili.
.
Kitendo cha kikundi cha watu kuzuia timu isiingie uwanjani kufanya mazoezi kwa mujibu wa kanuni na hatimaye kuathiri mchezo na kujenga picha mbaya kwa mashabiki, wadau na hata wafuatiliaji wa ligi yetu kinaonyesha wazi ni namna gani tunaiweka rehani hadhi tuliyopewa ya kutambulika kwa ligi hii kimataifa
.
Vitendo kama hivyo vinapaswa kulaaniwa vikali na mamlaka husika zichukue hatua madhubuti ili kudhibiti hali hiyo. Si hilo tu, bali makomandoo wa klabu hizo wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya kudhibiti na hata kuzima uhuru wa vyombo vya habari, jambo ambalo linakwenda kinyume na misingi ya uwazi na maendeleo ya soka. Kwa mfano, wamekuwa wakizuia waandishi kufanya mahojiano na viongozi wa timu na hata wachezaji.
.
Hivi Simba na Yanga kwa viwango zilipofikia zinastahili kweli kuwa na watu wa namna hii katika ulimwengu wa soka ambao umetawaliwa na mafanikio na burudani uwanjani. Zaidi ya hayo, makomandoo wengi hujihusika na vitendo vya vurugu na uonevu, hasa katika mechi kubwa kama Kariakoo Dabi. Matukio kama kuzuia wapinzani kutumia miundombinu ya umma kwa ajili ya maandalizi ya mechi ni dalili kwamba timu hizi kubwa bado zinakumbatia ukal? flani katika suala la ulinzi..