Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

SIMULIZI: JITU LA MSITUNI MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY) WHATSP: 0786978618 KITU KIPYAA Sehemu ya Kwanza

18th Apr, 2025 Views 26

SIMULIZI: JITU LA MSITUNI
MTUNZI: MAULID KIFUMBE (MR ROY)
WHATSP: 0786978618

KITU KIPYAA

Sehemu ya Kwanza

Msitu wa Giza ulikuwa maarufu kwa jina lake kutokana na giza nene lililotanda hata mchana wa jua kali. Ulikuwa msitu uliopo kaskazini mwa kijiji cha Mwibanza, eneo lililojaa miti mikubwa na wanyama wa kila aina. Lakini kilichofanya msitu huu utishe ni hadithi za wenyeji kuhusu kiumbe kikubwa, chenye manywele mengi, makucha marefu, na sura ya kutisha yenye macho mekundu kama makaa ya moto. Wenyeji walikijua kama Jitu la Msituni, na jina lake halisi lilijulikana kuwa ni Mkaboko.

Jitu hili lilisemekana kutokea mbali, kwenye milima ya Bahati, likikimbia jamii yake baada ya kutengwa kwa sababu ya ukubwa na ukatili wake. Watu walisimulia kwamba Mkaboko alizaliwa na nguvu za ajabu, lakini alikuwa mwenye hasira zisizodhibitika. Katika hali ya kutafuta mahali pa kujificha, Mkaboko aliingia Msitu wa Giza na kuutwaa kama maskani yake.

Mkaboko hakuwa binadamu wa kawaida. Hakuwa na mahali alikokubalika, kwani kila mahali alipokanyaga watu walitoweka au kuuliwa. Ukatili wake ulizidi pale alipokosa marafiki na familia ya kumuunga mkono. Msitu wa Giza ulikuwa kimbilio lake pekee, mahali ambapo hakuna mtu aliyethubutu kuingia kwa sababu ya giza na wanyama wakali waliouzunguka.

Lakini, Mkaboko hakuwa tu anataka kimbilio, bali pia alihitaji mahali pa kuonyesha uwezo wake wa kutisha. Msitu huo ulijaa uwindaji wa wanyama wa kila aina, chakula kilichomtosheleza, na giza lililosaidia kujificha na kuwinda binadamu wachache waliothubutu kuingia.

Mkaboko hakuwa anaua kwa njaa pekee, hasira zake za kupuuzwa na jamii ndizo zilizokuwa chanzo kikubwa. Kila mtu aliyethubutu kuingia msituni, hata kwa bahati mbaya, alihesabika kama mvamizi wa himaya yake. Aliona mauaji kama njia ya kulinda mipaka yake. Mwili wa binadamu kwake ulikuwa ushindi wa kijeshi. Waliovamia walikatwa vipande na viungo vyao vilifanywa onyo kwa wengine kwa kuvining’iniza juu ya miti mikubwa.

Mkaboko alijimilikisha Msitu wa Giza, wenye ukubwa wa hekta elfu mbili, uligeuka kuwa himaya ya Mkaboko. Hakuna mtu aliyethubutu kuingia bila taarifa za kupotea au kuuawa. Maisha ya viumbe wengine msituni pia yalidhibitiwa na Mkaboko, akifukuzana na wanyama wakali kama simba, fisi, na nyoka wakubwa ili kuwaonesha kwamba yeye ndiye bwana wa msitu huo.

Katika kijiji cha Mwibanza mbali na eneo hilo. Lakini kwa upande wa mjini, kulikuwa na kundi la watafiti waliovutiwa na msitu huu, wakiwa hawajui visanga vya msitu ule. Ndani ya chuo maarufu cha utafiti wa madawa, kiongozi wao Dr. Denis aliamua kuongoza timu kwenda kwenye msitu huo kufanya utafiti wa kisayansi.

Kwa miaka mingi, msitu huo uliendelea kutisha na kiumbe kikubwa, Mkaboko, aliendelea kutawala kwa amani. Lakini mpango wa Dr. Denis na timu yake ya watafiti ulikuwa unakaribia kuivuruga amani hiyo. Safari yao kuelekea Msitu wa Giza ilikuwa imeanza, na hata wakiwa hawajafika, hawakujua kuwa hatima yao ilikuwa mikononi mwa jitu la kutisha, Mkaboko.

Jua lilikuwa limeanza kuchomoza nyuma ya milima wakati msafara wa watafiti ulipoanza safari yao kuelekea Msitu wa Giza. Wakiongozwa na Dr. Denis, kundi hilo lilijumuisha wanafunzi wake saba, wakiwemo Rashid, Priska, Monica, na wengine. Kila mmoja alikuwa na sababu yake ya kujiunga kwenye safari hii, lakini lengo kuu lilikuwa kupata mimea ya nadra inayosemekana kuwa dawa ya magonjwa sugu.

Wakiwa ndani ya gari mbili za utafiti, kila mmoja alikuwa na furaha tele. Kicheko, nyimbo, na vichekesho vilitawala huku wakipita barabara ya vumbi kuelekea kwenye msitu huo wa kutisha. Rashid, mcheshi wa kundi hilo, alikuwa akiwaburudisha wenzake kwa hadithi zake za kubuni, huku akimfanya Priska, aliyekuwa mpole na mwenye aibu, kucheka kwa mara ya kwanza siku hiyo.

Lakini katikati ya furaha hiyo, Dr. Denis alikuwa kimya. Uso wake ulikuwa umejawa na mawazo mazito. Alikuwa akisoma ramani ya msitu huo na maandiko yaliyowatahadharisha kuhusu hatari zilizokuwepo. "Huu si msitu wa kawaida," alisema kwa sauti ya chini, lakini hakuna aliyemsikia.

Walipokaribia msitu huo, hali ya hewa ilibadilika ghafla. Upepo baridi ulianza kuvuma, na sauti za ndege wa porini zilianza kusikika kwa mbali. Miti mirefu iliyojaa majani mazito ilianza kuonekana, ikifunika mwanga wa jua na kutengeneza kivuli kizito hata wakati wa mchana.

Waliposhuka kwenye magari, Monica, mpenzi wa Dr. Denis, alihisi hofu kwa mara ya kwanza. "Denis, kweli tunaweza kuingia humo?" aliuliza kwa sauti ya wasiwasi.
"Ni lazima, Monica. Tumekuja kwa sababu ya utafiti huu, na hatuwezi kurudi mikono mitupu," Dr. Denis alijibu kwa uthabiti.

Kila mmoja alivaa vifaa vya utafiti kofia za chuma, viatu vizito vya msituni, na mikoba iliyojaa zana mbalimbali. Walianza safari ya kuingia msituni huku wakifuatilia alama walizoweka kwenye ramani yao.

Msitu ulizidi kuwa wa kutisha kadri walivyoingia ndani. Nyoka wakubwa walionekana kupita katikati ya nyasi, na wadudu wakali waliwazunguka kila kona. Priska, ambaye alikuwa na hofu ya nyoka, alishika mkono wa Rashid kwa nguvu, akimfanya Rashid ajisikie ujasiri wa kumlinda.

Walifika eneo ambalo ramani ilionyesha kuwa ndilo lilikuwa na mimea ya dawa waliyoitafuta. Walianza kukagua kila kona ya msitu huku wakibadilishana mawazo kwa furaha. "Hii ni mimea ya nadra sana," alisema Monica, akiandika maelezo kwenye daftari lake.

Lakini hawakujua kwamba walikuwa wamekaribia eneo lililokuwa nyumbani kwa Mkaboko, Jitu la Msituni. Kwa mbali, macho mekundu yalikuwa yakiwatazama kwa hasira. Kiumbe hicho kikubwa kilikuwa kimejificha juu ya mti mkubwa, kikisikiliza na kuangalia kila hatua yao.

Katika harakati zao za kuchunguza msitu, walikanyaga nyayo kuelekea kwenye eneo lililojaa majani yaliyopangwa kwa namna ya kipekee. Kwa bahati mbaya, walikuwa wdamevamia nyumba ya Mkaboko bila kujua. Rashid alisimama kwa mshangao!. "Inaonekana hapa kuna kitu cha ajabu."
"Ni lazima tuangalie," Dr. Denis aliamuru, bila kujua kwamba walikuwa wamevuka mpaka wa hatari.

Waliendelea kuzunguka eneo hilo, wakiangalia mabaki ya mifupa ya wanyama na vitu vilivyoonekana kama silaha za kizamani. Hakuna aliyegundua kwamba Mkaboko alikuwa amewalenga. Hasir1a zake ziliongezeka alipowaona wakivamia eneo lake la faragha.

Msitu ulizidi kuwa wa kutisha, na ukimya wa ghafla ulianza kuwatisha watafiti hao. Bila kujua, walikuwa wamechochea hasira za kiumbe ambacho hakihitaji sababu kubwa kuua. Mkaboko alianza kufuata nyayo zao kwa ukimya, akijipanga kwa uvamizi.

LIPIA BUKU 1000, NIKUTUMIE STORY HII, NIKIONA MUAMALA NAINGIA KUKUTUMIA.
NAMBA ZA MALIPO
M PESA: 0741278618
JINA: MBASHIRU HAMZA MUSSA.

AIRTEL MONEY: 0786978618
JINA: FATUMA MAULID KWANAMA

JIUNGE KWENYE HILI GROUP LANGU LA WHATSP USOME STORY ZANGU.??
https://chat.whatsapp.com/I3DNSQcYYxO8qpkUTpIlNq.

Za hivi punde ni za 🔥🔥🔥 | Sema Jambo
Your settings were saved successfully!
Something went wrong!
You're not logged in
Click here to login and post your story

Welcome gonga94 Continue reading the various stories available here. Click here. Are you an artist then create an account here Signup/Login


mjukuu rewards 100
 

NITAKUPA USINIROGE (1)

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 19

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 18

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 17

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 16

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 42

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 41

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 40

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 39

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 38

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 37

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 36

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 35.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 34

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 33.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 32

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 31

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 30

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 29

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 28

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 27

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 26

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 25

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 24

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 23.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 22

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 21

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 20

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 19.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 18

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 17.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 16

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 15.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 14

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 13.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 12

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 11.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 10

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 09

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 08

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 07.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 06

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 05.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 04.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 03

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 02

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 01.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 22.

mjukuu rewards 0
 

NASEMA KWA MAMA **** 3--4

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 15

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 14

mjukuu rewards 0
 

WIFI KHAA 04

mjukuu rewards 0
 

NASEMA KWA MAMA* 1-----2

mjukuu rewards 0
 

KIJIJI CHA WAGENI! 04

mjukuu rewards 0
 

MKE WA MGANGA ( 1——5 )

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 13

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 21.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 20.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 19.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 18.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 17.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 16.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 15.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 14.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 13.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 12.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 11

mjukuu rewards 0
 

WIFI KHAA 02 #Tulipoishia

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 10

mrindia rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 09

mjukuu rewards 0
 

*MY CHUNUN* 01

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 09

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA. EP: 08

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP 07

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP 06

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP 05

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA. EP: 4

mjukuu rewards 0
 

SHANGATISA EP: 3

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: {02}

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA. EP: 1

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 08

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU (06 & 07)

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 05

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 04

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 03

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU (01& 02)

mrindia rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 01

mjukuu rewards 0
 

MTOTO WA GETI KALI 1 - 6

mjukuu rewards 0
 

MIMI SIO KICHAA

mrindia rewards 0
 

SITOMWACHA HATA IWEJE

mjukuu rewards 0
 

BINTI MCHAWI

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest