? CONFIRMED: Bodi ya Ligi Kuu imethibitisha kupitia Kamati yake ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kuwa imeamua kuahirisha mchezo wa Derby ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba kwa mujibu wa Kanuni ya 34:1(1.3) ya Ligi Kuu kuhusu Kuahirisha Mchezo, ili kutoa nafasi ya kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kufanya maamuzi ya haki.
.
Bodi imeeleza kuwa itatoa taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo na kutangaza tarehe ya mchezo huo mapema iwezekanavyo..