KARIAKOO DERBY: Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuahirisha mechi ya ‘dabi’ ya Kariakoo ambayo ilipangwa ichezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa.
Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, kuahirishwa kwa mechi hiyo kumekuja baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Kuu Tanzania, kupitia shauri la klabu ya Simba kuzuiliwa kuingia katika dimba la Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya leo kuvaana na wenyeji wao Yanga SC.
“Bodi ilipokea taarifa ya afisa usalama wa mchezo huo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyoambatana na tukio la Simba kushindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati”, imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema, bodi imeahirisha mchezo huo ili kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kufanya maamuzi ya haki.
#NBCPremierLeague #NBCPL #KariakooDerby #WataniWaJadi #YangaSimba #YangaSC #SimbaSC #HainaKipengele.