Hili ni neno jingine usilotakiwa kulitafuta kule Google. Neno hilo limebeba maudhui ya maiti za watu waliouliwa na mikono ya Serial Killer mmoja aliyewahi isumbua sana nchi ya Urusi.
Huyu jamaa aliitwa Andrei Chikatilo. Watu wengine bwana sijui huwa wameumbwaje tu. Chikatilo katika maisha yake alifanya mauaji ya watu 50. Lakini tofauti na wale Manson Family - huyu jamaa wengi katika wahanga wake walikua ni wanawake na watoto.
Historia inamjua kama moja ya wauaji katili sana. Chikalito alizaliwa Ukraine mwaka 1936, ambayo kwa wakati huo ilikua ni sehemu ya Umoja wa Kisovieti. Kurasa za historia hazina nakala nyingi zinazoelezea nyakati za furaha katika maisha ya Chikatilo. Huyu jamaa alizaliwa na kukuzwa katika kile kipindi cha njaa kali iliyowahi ikumba nchi ya Urusi. Kuna tetesi ingawa zinafichwa sana, zinadai kuwa….