Kwa chuki waliyokuwa nayo Familia ya Manson. Baada ya kufanya mauaji waliandika maneno mbalimbali ukutani, moja wapo likiweno ni neno “Death to Pigs” - kauli ambayo inahusishwa na chuki binafsi ambazo zaweza kuwa ni chuki dhidi ya kabila, dini au rangi. Maneno haya ukutani yaliandikwa kwa damu.
Kwa juhudi za polisi. Manson na wafuasi wake walikamatwa. Manson alipandishwa kizimbani mwaka 1971 ambapo alikutana na adhabu ya kifo. Adhabu ambayo hata hivyo hakuitumikia kwasababu, adhabu hiyo ilibadilishwa kuwa kifungo cha maisha gerezani baada ya Mahakama jimbo la California, Marekani kuifuta adhabu ya kifo mwaka 1972. Manson alifariki mwaka 2017 akiwa na miaka 83. Baadhi ya wafuasi waliokua chini yake bado wako gerezani hadi leo hii..