Manson ambaye historia yake imejaa kumbukumbu za kuingia jela na kutoka. Alisifika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kushawishi. Na hii ndio sababu alikua na vijana wengi waliomfata kila alichosema kama mtume. Lakini usichokijua kuhusu mauaji ya Tate-LaBianca Killings ni kuwa…
Manson na kundi lake wanadaiwa walifanya mauaji yale wakisukumwa na chuki za kikabila. Sasa kama wewe ulidhani ukabila upo kule kwa Wakulima na Wafugaji pekee. Nikwambie tu haya mambo yapo hadi huko uzunguni paliko endelea.
Usiku wa kati ya tarehe 8 na 10, Manson na kundi lake walifanya moja ya matukio mabaya kuwahi kufanywa Marekani. Waliua watu watano wa familia moja. Na ishu haikua kuwaua pekee. Ishu inakuja kwa namna walivyowaua. Wahanga walichinjwa na kukatwa mapanga, huku pia maiti zao zikikutwa na majeraha ya visu maeneo mbalimbali ya miili yao. Lakini hilo halikutosha….