Tukio la 1 ni “Tate-LaBianca Killings – 1969”
Hili tukio linahusisha mauaji ya kinyama ambayo maarufu yanajulikana kama LaBianca Murders.
Haya mauaji yalitokea kati ya Agosti 8 na 10 mwaka 1969. Taarifa rasmi kuhusu kilichotokea zinasema, watu watano waliuliwa vibaya na wanachama wa kundi la "Manson Family."
Lakini kwanza…
Naomba usiwachanganye Freemasons na hii familia ya Manson. Wanaweza kuwa wamefanana ama hawajafanana kimatukio. Huu ukweli hapa tutakuja ujua kwenye Story zinazokuja. Lakini…
Familia ya Manson ni jina tu lililopewa kundi la wahuni waliokuwa wakiishi pamoja chini ya uongozi wa Charles Manson mwishoni mwa miaka ya 60 huko California, Marekani. Kundi hili lilikuwa na mchanganyiko wa vijana ambao ni kama walikua vichaa wanaomuabudu kiongozi wa familia hiyo, bwana Manson..